
Location:
New Rochelle, NY
Genres:
News & Politics Podcasts
Networks:
United Nations
Description:
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Twitter:
@HabarizaUN
Language:
Swahili
Contact:
9178215291
14 MEI 2026
5/14/2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW70 uliofanyika mwezi Machi mwaka huu hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo tulipata fursa ya kuzungumza na washiriki wakiwemo wawakilishi wa mashirika ya wanawake. Miongoni mwao ni Severina Lemachokoti kutoka asasi ya kiraia ya Naretu Girls and Women Empowerment Programme iliyoko kaunti ya Samburu nchini Kenya, ambaye katika mahojiano na Flora Nducha ameelezea jinsi mila na desturi kwa wanawake na wasichana kutorithi chochote kwenye jamii yao zinavyoanza kuyoyoma. Pia tunamsikia kutoka Salome Gatakaa Araka wa FODDAJ ambalo ni Jukwaa la Maendeleo ya Wanawake, Demokrasia na Haki, nchini Kenya ni shirika la kiraia ambalo mwaka huu kwa mara nyingine lilishiriki mkutano huo wa CSW70. Baada ya kushriki vikao mmoja wa viongozi wa shirika hilo amezungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa na ndio msingi wa mahojiano haya.Tunakuletea pia muhtasari wa habari zikiwemo za hali ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na Sudan, pamoja na masuala ya afya tukimulika yanaoendelea kuhusu virusi vya Hanta au Hantavirus.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Duration:00:09:58
Katibu Mkuu Antonio Guterres aaga Muungano wa Afrika na kutoa tathmni ya ushirikiano wa UN-AU
5/13/2026
Huu ndio mkutano wangu wa mwisho kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema António Guterres, baada ya mkutano wa 10 wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa hii leo huko Addis Ababa, Ethiopia, huku akijinasibu kuwa ushirikiano kati ya vyombo hivyo wakati wa kipindi chake cha miaka 10 umekuwa moja ya mifano imara ya ushirikiano thabiti wa kimataifa.. Assumpta Massoi anafafanua zaidi kwenye taarifa hii.
Duration:00:02:33
13 MEI 2026
5/13/2026
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa António Guterres hii leo huko Addis Ababa nchini Ethiopia, wanawake wanaowasili Ulaya kufuatia ukeketaji wa lazima katika nchi zao, na mafunzo ya kutatua migogoro kwa njia mbadala Zanzibar.Huu ndio mkutano wangu wa mwisho kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema António Guterres, baada ya mkutano wa 10 wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa hii leo huko Addis Ababa, Ethiopia, huku akijinasibu kuwa ushirikiano kati ya vyombo hivyo wakati wa kipindi chake cha miaka 10 umekuwa moja ya mifano imara ya ushirikiano thabiti wa kimataifa.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania, limetoa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wa kutatua migogoro kwa njia mbadala (ADR), wasaidizi wa kisheria 126 kutoka kisiwani Pemba, Zanzibar ili kusogeza huduma za kisheria karibu na jamii na kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani.Wanawake wengi wahamiaji na wakimbizi kutoka Afrika wanaowasili barani Ulaya wakisaka usalama na maisha bora hujikuta wakikabiliwa na majeraha ya kiwewe, changamoto za lugha na kutengwa kijamii. Nchini Ujerumani, shirika lililoanzishwa na wakimbizi, la AfroKids International, linafanya kazi ya kuwapa matumaini na msaada wanawake hao, hususan manusura wa ukeketaji au FGM. Akizungumza na Flora Nducha Idhaa hii kandoni mwa mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 uliomalizika mwezi uliopita hapa Umoja wa Mataifa, Farina Gorma afisa mkuu wa shirika hilo la kimataifa katika ofisi ya Stuttgart amesema wanawake wengi wanaowasili Ulaya hukumbana na mtihani hasa wa kupata huduma za afya, msaada wa kisheria na usaidizi wa kisaikolojia..Mwenyeji wako ni Anold Kayandai, karibu!
Duration:00:09:59
UNDPTanzania yajengea uwezo wasaidizi wa kisheria 126 kisiwani Pemba, ili kutatua migogoro kwa njia mbadala
5/13/2026
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania, limetoa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wa kutatua migogoro kwa njia mbadala (ADR), wasaidizi wa kisheria 126 kutoka kisiwani Pemba, Zanzibar ili kusogeza huduma za kisheria karibu na jamii na kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani. Rashid Malekela na taarifa zaidi.
Duration:00:02:48
AfroKids International ni tumaini kwa wanawake wakimbizi barani Ulaya - Farina
5/13/2026
Wanawake wengi wahamiaji na wakimbizi kutoka Afrika wanaowasili barani Ulaya wakisaka usalama na maisha bora hujikuta wakikabiliwa na majeraha ya kiwewe, changamoto za lugha na kutengwa kijamii. Nchini Ujerumani, shirika lililoanzishwa na wakimbizi, la AfroKids International, linafanya kazi ya kuwapa matumaini na msaada wanawake hao, hususan manusura wa ukeketaji au FGM. Akizungumza na Flora Nducha Idhaa hii kandoni mwa mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 uliomalizika mwezi uliopita hapa Umoja wa Mataifa, Farina Gorma afisa mkuu wa shirika hilo la kimataifa katika ofisi ya Stuttgart amesema wanawake wengi wanaowasili Ulaya hukumbana na mtihani hasa wa kupata huduma za afya, msaada wa kisheria na usaidizi wa kisaikolojia.
Duration:00:03:19
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno “Payapaya.’’
5/12/2026
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania anafafanua maana ya neno “Payapaya.’’
Duration:00:01:02
12 MEI 2026
5/12/2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Côte d'Ivoire ambako wakulima wameshuhudia kuimarika taratibu kwa uzalishaji wa kakao baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kusaidia wakulima nchini humo kurejesha ardhi katika ubora wake na kuongeza uzalishaji kupitia mbinu endelevu za kilimo mseto cha misitu, mazao na mifugo..Afrika imekuwa mstari wa mbele kushinikiza mfumo mpya wa kifedha unaozingatia usawa kwa nchi zinazoendelea. Na leo katika mkutano wa kuangazia mustakbali wa Afrika, Africa Forward huko Nairobi nchini Kenya, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amezipongeza nchi za Afrika kwa kuongoza juhudi hizo za mageuzi ya mifumo ya fedha duniani. Kuhusu utajiri wa madini yanayopatikana Afrika kunufaisha nchi nyingine nje ya bara hilo Guterres amesema “Hakuna tena unyonyaji wala uporaji. Watu wa Afrika lazima wanufaike kwanza, na zaidi kutokana na rasilimali za Afrika.”.Taarifa mpya kuhusu virusi vya hanta ni kwamba hadi sasa wagonjwa walioripotiwa ni 11, na watu watatu wamefariki dunia. Kati ya wagonjwa hao, tisa wamethibitishwa kuwa na virusi vya Andes huku wawili wakihesabika kuwa wagonjwa wanaoshukiwa lilesema shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO. WHO pia wameipongeza serikali ya Hispania kwa ushirikiano wake katika mchakato mzima wa kuwaondoa salama na kuwarejesha makwao abiria takriban 150 kutoka nchi 23 waliokuwa katika meli ya kitalii ya MV Hondius ambapo humo ndio mlipuko wa hanta ulipotokoea.ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa hivi karibuni kuhusu Malengo ya Misitu Duniani, Global Forest Goals kwa mwaka 2026 ikieleza bayana kuwa misitu ina mchango mkubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuhifadhi bioanuwai, kuimarisha uhakika wa chakula na kusaidia maisha ya mamilioni ya watu duniani. Nchini Kenya mkazi mmoja ameeleza bayana jinsi wanavyonufaika na msitu asili wa Ngong ulioko takribani kilometa sita kutoka mji mkuu Nairobi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania anafafanua maana ya neno “Payapaya’’Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Duration:00:09:58
Akili Mnemba au AI haiwezi kuchukua nafasi ya kuwa mama
5/11/2026
Je Akili mnemba AI inaweza kuchukua ajira yako? Ingawa kila uchwao AI inaandika upya sheria za kazi, ubunifu na kubadili vile tunavyoishi lakini kuna kazi moja ambayo bado watu wanasema hiyo ni ya watu maalum sana na kwamba AI haiwezi kuichukua. Hapo jana jumapili tarehe 10 Mei dunia iliadhimisha siku ya wakina mama duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya Uzazi UNFPA lilitembelea viunga vya New York Marekani na kuzungumza na wanawake. Tuungane na Leah Mushi kusikia wamesema nini kuhusu AI.
Duration:00:03:03
Siku ya Kinamama: Mama ni nguzo ya jamii na msingi wa haki za watoto
5/11/2026
Je wajua nafasi ya mama katika jamii? Dunia ikiwa imeadhimisha siku ya mama Jumapili Mei 10, tunakupeleka kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambako nafasi mama ya katika kusongesha haki za kijamii hususan za watoto wao imewekwa bayana. Feissal Kirwa anafafanua kwenye taarifa hii itokanayo na video iliyoandalaliwa na Redio washirika wetu Domus.
Duration:00:02:42
11 MEI 2026
5/11/2026
Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres nchini Kenya, Akili Mnemba katika nafas iza ajira, na nafasi ya mama katika jamii ikiturejesha nchini Kenya kusikiliza simulizi za wamama.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres yuko ziarani nchini Kenya kushuhudia uwekezaji mkubwa wa Umoja wa Mataifa wenye thamani ya karibu dola milioni 340 katika makao yake makuu jijini Nairobi. Uwekezaji huo unaelezwa kuwa moja ya miradi mikubwa zaidi ya miundombinu ambayo Umoja wa Mataifa umewahi kufanya barani Afrika.Je Akili Mnemba, AI inaweza kuchukua ajira yako? Ingawa kila uchwao AI inaandika upya sheria za kazi, ubunifu na kubadili vile tunavyoishi lakini kuna kazi moja ambayo bado watu wanasema hiyo ni ya watu maalum sana na kwamba AI haiwezi kuichukua. Hapo jana jumapili tarehe 10 Mei dunia iliadhimisha siku ya wakina mama duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya Uzazi UNFPA lilitembelea viunga vya New York Marekani na kuzungumza na wanawake.Je wajua nafasi ya mama katika jamii? Dunia ikiwa imeadhimisha siku ya mama Jumapili Mei 10, tunakupeleka kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambako nafasi mama ya katika kusongesha haki za kijamii hususan za watoto wao imewekwa bayana. Feissal Kirwa anafafanua kwenye taarifa hii itokanayo na video iliyoandalaliwa na Redio washirika wetu Domus.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Duration:00:11:21
UN yawekeza dola milioni 340 Nairobi kuimarisha kitovu chake barani Afrika
5/11/2026
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres yuko ziarani nchini Kenya kushuhudia uwekezaji mkubwa wa Umoja wa Mataifa wenye thamani ya karibu dola milioni 340 katika makao yake makuu jijini Nairobi. Uwekezaji huo unaelezwa kuwa moja ya miradi mikubwa zaidi ya miundombinu ambayo Umoja wa Mataifa umewahi kufanya barani Afrika. Stella Vuzo kutoka kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi anafuatilia zira hiyo na hii hapa taarifa yake.
Duration:00:04:02
08 MEI 2026
5/8/2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Kigoma nchini Tanzania tunamsikia Mwakilishi Mkazi wa FAO Tanzania Nyabenyi Tito Tipo ambaye alitembelea mkoa huo kuona hali ya utekelezaji na mgao wa vifaa vya kuimarisha sekta ya uvuvi. Pia tunakuletea muhtasari wa habariShirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO limesema Virusi ya Hanta havifanani na vya COVID na kwamba wanaelewa bado watu wana kumbukumbu mbichi za ugonjwa huo. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi msemaji wa WHO Christian Lindmeier amesema wanaendelea kuratibu na kufuatilia kwa karibu mlipuko wa ugonjwa huo uliotokea kwenye meli ya kifahari ya kitalii na kwamba “Hatari ni ndogo kabisa, hii si COVID mpya.”Matthew Hollingworth ambaye ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani (WFP) amerejea hii leo kutoka Somalia na kuwaeleza waaandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi yale aliyojionea akiwa ziarani nchini humo kwa wiki moja kuwa “ Nimeona familia ambazo zimeshuhudia madhara mengi kwa wakati mmoja ikiwemo athari za hali mbaya ya hewa, migogoro na shinikizo la kiuchumi, athari zote hizo zimekuwa zikisukuma njaa hadi katika viwango vya hatari .”Na, Wanawake na wasichana nchini Lebanon wanaendelea kuuawa, kujeruhiwa na kukimbia makazi yao licha ya makubaliano dhaifu ya usitishaji mapigano yaliyoanza kutekelezwa Aprili 17 mwaka huu, limeonya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake UN Women.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Duration:00:10:55
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "MKUNGUNI."
5/7/2026
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKUNGUNI."
Duration:00:00:29
07 MEI 2026
5/7/2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo kandoni mwa kikao cha UNPII Flora Nducha alizungumza na mshiriki kutoka Tanzania kwenye jamii ya Wamaasai mwana harakati wa haki za jamii hiyo Adam Kulet Ole Mwarabu aliyeanza kwa kumueleza kwanini mwaka huu ni wa kipekee kwa watu wa jamii za asili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na neno la wiki.Siku ya tano tangu kuripotiwa kwa virusi vya Hanta kwenye meli ya kifahari ya Hondius kutoka Argentina na kulazimika kutia nanga nchini Cabo Verde, hii leo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, (WHO) Dkt. Tedros Ghebreyesus amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kuwa uchunguzi kuhusu mlipuko huo uliosababisha hadi sasa vifo vya watu 3 wakiwemo wanandoa wawili unaendelea.Tukisalia na mlipuko huo wa virusi vya Hanta, Mwakilishi wa WHO nchini Cabo Verde amesema hivi sasa meli hiyo Hondius iko njiani kuelekea visiwa vya Canary nchini Hispania, “na kwenye meli tuna daktari wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kuna madaktari wawili wa Kiholanzi ambao wameimarisha timu, na kuna mtaalamu mmoja wa magonjwa ya mlipuko ambaye atasafiri na meli hadi bandari inayofuata ambayo ni visiwa vya Canary. Kwa sasa hakuna mtu mgonjwa kwenye meli, lakini iwapo mtu ataugua, basi kutakuwa na madaktari na vifaa vya matibabu vya kuwahudumia wakati wa safari.”Nchini Tanzania hivi karibuni ripoti ya uainishaji wa viwango vya upatikanaji wa chakula nchini humo iliyoandaliwa kwa pamoja na serikali na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO ilieleza kuwa baadhi ya maeneo ya Halmashauri za wilaya za Same, Maswa na Monduli yako katika kiwango cha tatu yaani (IPC 3).Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKUNGUNI"Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Duration:00:09:59
Miaka 25 ya Jukwaa la Watu wa Asili Tanzania imepiga hatua kutujumuisha - Ole Kulet Mwarabu
5/7/2026
Haki ya afya kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ni haki ya kila mtu bila kujali uko kwenye kundi au jamii gani. Huo ulikuwa ni msisitizo mwaka huu kwenye Jukwaa la jamii za watu wa asili lililokuja jamvi wiki iliyopita hapa New York Marekani. Na kandoni mwa kikao hicho Flora Nducha alipata fursa ya kuzungumza na mshiriki kutoka Tanzania kwenye jamii ya Wamaasai mwana harakati wa haki za jamii hiyo Adam Kulet Ole Mwarabu aliyeanza kwa kumueleza kwanini mwaka huu ni wa kipekee kwa watu wa jamii za asili
Duration:00:08:12
Serikali ya Tanzania inajali usawa na haki kwa watu wote kupata huduma kwa usawa - Profesa Malebo
5/6/2026
Siku tano zilizopita Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefunga pazia hapa katika makao ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani baada ya majadiliano ya takribani wiki mbili ya wadau kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera, mafanikio na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuhudumia wananchi wao ikiwemo jamii za watu wa asili. Kwa upande wa Tanzania, mmoja wa walioshiriki ni Katibu Mtendaji wa Tume ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ya Taifa la Tanzania, Profesa Hamisi Masanja Malebo.Feisal Kirwa wa idhaa hii alifanya mahojiano naye kwanza akitaka kufahamu Tanzania ina mikakati gani ya kuhakikisha watu wa asili wanajumuishwa katika huduma za afya kwa wote?
Duration:00:02:34
Abiria mwingine amethibitishwa kuwa na ugonjwa wa virusi vya Hanta
5/6/2026
Imethibitishwa kuwa abiria mwingine aliyekuwa kwenye meli ya kitalii iliyohusishwa na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Hanta au Hantavirus ameambukizwa ugonjwa huo, ugonjwa ambao tayari umeua watu watatu waliokuwa ndani ya meli na kusababisha tahadhari ya kimataifa iliyoratibiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) la Umoja wa Mataifa. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.
Duration:00:02:35
06 MEI 2026
5/6/2026
Hii leo jaridani tunaangazia maambukizi wa Hantavirus, juhudi za kutokomeza Adhabu za Viboko shuleni nchini Tanzania, na ujumbe wa Profesa Hamisi Masanja Malebo kuhusu haki za watu wa asili.Imethibitishwa kuwa abiria mwingine aliyekuwa kwenye meli ya kitalii iliyohusishwa na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Hanta au Hantavirus ameambukizwa ugonjwa huo, ugonjwa ambao tayari umeua watu watatu waliokuwa ndani ya meli na kusababisha tahadhari ya kimataifa iliyoratibiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) la Umoja wa Mataifa.Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko huadhimishwa Aprili 30 ya kila mwaka, na mwaka huu katika maadhimisho ya siku hiyo wiki iliyopita, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF, nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa haki za binadamu na elimu lilizindua kampeni iitwayo ‘No Collabo’ iliyolenga kukomesha adhabu ya viboko kwa mtindo ambao walimu zaidi ya mmoja humchapa mwanafunzi viboko kwa wakati mmoja. Rashid Malekela amezungumza na wazazi mkoani Mwanza Kaskazini Magharibi mwa nchini hiyo kupata maoni yao.Siku tano zilizopita Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefunga pazia hapa katika makao ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani baada ya majadiliano ya takribani wiki mbili ya wadau kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera, mafanikio na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuhudumia wananchi wao ikiwemo jamii za watu wa asili. Kwa upande wa Tanzania, mmoja wa walioshiriki ni Katibu Mtendaji wa Tume ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ya Taifa la Tanzania, Profesa Hamisi Masanja Malebo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Duration:00:09:59
UNICEF Tanzania yaongoza kampeni kukomesha adhabu ya viboko shuleni
5/6/2026
Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko huadhimishwa Aprili 30 ya kila mwaka, na mwaka huu katika maadhimisho ya siku hiyo wiki iliyopita, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF, nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadauwa haki za binadamu na elimu lilizindua kampeni iitwayo ‘No Collabo’ iliyolenga kukomesha adhabu ya viboko kwa mtindo ambao walimu zaidi ya mmoja humchapa mwanafunzi viboko kwa wakati mmoja. Rashid Malekela amezungumza na wazazi mkoani Mwanza Kaskazini Magharibi mwa nchini hiyo kupata maoni yao.
Duration:00:03:09
Jifunze Kiswahili: Maana ya methali “Kwendako mema hurudi mema."
5/5/2026
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kwendako mema hurudi mema."
Duration:00:01:02